Nyakati za mlindimo zimerudi tena katika bonde la Silikoni. Maegesho ya barabara kuu ya 101 yamepambwa tena na nakshi za waanzilishi wenye matumaini. Nyumba za kupanga zimefurika, ikiwa ni uhitaji wa nyumba za kifahari katika miji ya mapumziko kama ziwa Tahoe, ikiwa ni dalili ya ongezeko la baraka. Eneo la Ghuba lilikuwa kitovu cha tasnia hii ya mpito na mashirika ya tarakilishi na mdahalishi ambayo yamekua katika mwamko wake. Sogora zake zilileta maajabu mengi ambayo yanafanya dunia ijisikie kuwa ya siku za usoni, kutoka simu za mpapaso mpaka utafiti wa muda mfupi sana wa maktaba kubwa katika kurusha kamera za angani kutoka umbali wa maili nyingi. Uhuisho katika shughuli zake za biashara tangu 2010 zinapendekeza kuwa maendeleo ni ufuatiliaji wake.
Hivyo, inaweza kuja kama mshangao kwamba baadhi ya watu katika bonde la Silikoni kudhani ya kuwa eneo hilo haliendelei, na ya kwamba kiwango cha uvumbuzi kimekuwa kikishuka kwa miongo mingi. Peter Thiel ambaye ni mwanzilishi wa Paypal, na mwekezaji wa nje wa kwanza katika Facebook,husema kuwa uvumbuzi katika nchi ya Marekani ni “Popote kati ya kuzama na kifo”. Wahandisi kutoka nyanja zote wanapatwa na hisia za nuhusi zinazofanana. Na kundi dogo lakini linalochipukia la wanauchumi linakadiria matokeo ya kiuchumi katika uvumbuzi wa sasa kuwa unaweza chuja kulinganisha na ule uliopita.
[ … ]
Kupitia bodi, uvumbuzi ambao umechochewa na umeme wa usindikaji wa bei nafuu unashika hatamu. Tarakirishi zinaanza kuelewa lugha za kawaida. Watu wanaongoza michezo ya runinga kwa kutumia mijongeo ya mwili tu – teknolojia ambayo inaweza pata matumizi sana katika ulimwengu wa kibiashara. Uchapaji wa pandeolwa-3 una uwezo wa kuleta mapokeo tete yanayoongezeka ya vitu, na inaweza kwenda hadi kwenye tishu za binadamu pamoja na nyenzo zingine za kikaboni.
Mchambuzi wa uvumbuzi anaweza puuza hii kama “msongamano wa kesho”. Lakini wazo la ukuaji unaoongozwa na teknolojia unatakiwa ama uendelee kutofungwa au kushuka kwa kasi, kuliko kudidimia na kuporomoka, kwani inakinzana na historia. Chad Syverson wa Chuo Kikuu cha Chicago anabainisha kwamba ukuaji wa uzalishaji wakati wa matumizi ya mwanzo ya umeme ulikuwa mzito. Ukuaji ulikuwa wa taratibu wakati wa majira ya uvumbuzi muhimu wa umeme mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20; kisha ulifurika.